Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 94

94
Mungu amlipiziaye mwenye haki
1Ee BWANA, Mungu wa kisasi,
Mungu wa kisasi, uangaze,
2 # Mwa 18:25 Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze,
Uwape wenye kiburi stahili zao.
3 # Ayu 20:5 BWANA, hadi lini wasio haki,
Hadi lini wasio haki watashangilia?
4 # Yud 1:15 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno,
Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?
5Ee BWANA, wanawaponda watu wako;
Wanautesa urithi wako;
6Wanamwua mjane na mgeni;
Wanawaua yatima.
7Nao husema, BWANA haoni;
Mungu wa Yakobo hatambui.
8Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini;
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?
9 # Kut 4:11; Mit 20:12 Aliyelitia sikio mahali pake, asisikie?
Aliyelifanya jicho, asione?
10 # Ayu 35:11; Yn 6:45; Isa 2:3; 28:26 Awaadibuye mataifa, asikemee?
Amfundishaye mwanadamu, asijue?
11 # 1 Kor 1:21; 3:20 BWANA anajua mawazo ya mwanadamu,
Ya kuwa ni ubatili.
12 # Ayu 5:17; Mit 3:11; 1 Kor 11:32 Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye,
Na kumfundisha kwa sheria yako;
13Ukimponya katika siku za shida,
Hadi asiye haki atakapochimbiwa shimo.
14 # Kum 31:6; 1 Sam 12:22; 1 Fal 6:13; Yer 31:37 Kwa kuwa BWANA hatawatupa watu wake,
Wala hutauacha urithi wake,
15Maana hukumu itarejea kwa wenye haki,
Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.
16Ni nani atakayesimama
Kwa ajili yangu juu ya wabaya?
Ni nani atakayenisaidia
Juu yao wafanyao maovu?
17Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,
Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.
18Niliposema, Mguu wangu unateleza;
Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza.
19Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu,
Faraja zako zinaifurahisha roho yangu.
20 # Amo 6:3; 2 Kor 6:14; Zab 58:2; Isa 10:1 Je! Watawala waovu wanaweza kushirikiana nawe,
Wale watungao madhara kwa njia ya sheria?
21 # Mt 27:1; Kut 23:7; Mit 17:15 Kwa pamoja wanaishambulia nafsi yake mwenye haki,
Na kuihukumu damu isiyo na hatia.
22Lakini BWANA amekuwa ngome kwangu,
Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia.
23 # Mit 2:22 Naye atawarudishia uovu wao,
Atawaangamiza katika ubaya wao,
Naam, BWANA, Mungu wetu, atawaangamiza.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 94: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia