Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 90

90
KITABU CHA NNE
Mungu adumuye milele na binadamu apitaye
Sala ya Musa, Mtu wa Mungu.
1Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,
Kizazi baada ya kizazi.
2 # Ayu 38:4-6; Mit 8:25 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3 # Mwa 3:19; Mhu 12:7 Wamrudisha mtu mavumbini,
usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4 # Ebr 13:8; 2 Pet 3:8 Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
5 # Isa 40:6 Wawafutilia wanadamu mbali kama ndoto,
wao ni kama majani yameayo asubuhi.
6 # Ayu 14:2; Zab 92:7 Asubuhi yachipuka na kumea,
Jioni yakatika na kukauka.
7Maana tumeangamia kwa hasira yako,
Na kwa ghadhabu yako tumezidiwa.
8 # Zab 50:21; Yer 16:17; Zab 19:12; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1 Kor 4:5; Ebr 4:12,13 Umeyaweka maovu yetu mbele zako,
Dhambi zetu za siri katika mwanga wa uso wako.
9Maana kwa hasira yako maisha yetu yanapita punde,
Maisha yetu yanaisha kama kite.
10Miaka ya maisha yetu ni sabini,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;
Tena kiburi chake ni taabu na ubatili,
Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
11Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?
Na ghadhabu yako inayolingana na kicho chako?
12 # Zab 39:4 Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
13 # Kum 32:36 Urudi, Ee BWANA utakasirika hadi lini?
Wahurumie watumishi wako.
14Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa,
Miaka sawa na ile tuliyopatwa na maovu.
16 # Zab 44:1; Hab 3:2 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,
Na utukufu wako kwa watoto wao.
17 # Isa 26:12; 2 The 2:16,17 Na fadhili za BWANA, Mungu wetu, ziwe juu yetu,
Na kazi ya mikono yetu uifanye thabiti,
Naam, kazi ya mikono yetu uifanikishe.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 90: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha