Zaburi 51:7-15
Zaburi 51:7-15 SRUV
Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya upendo. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na umwagaji wa damu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako. Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.