Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 44:1-8

Zaburi 44:1-8 SRUV

Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale. Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa, Ukawakalisha wao. Wewe uliwatesa watu wa nchi, Ukawafanikisha wao. Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao. Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu, Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo. Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu; Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao. Maana sitautumainia upinde wangu, Wala upanga wangu hauwezi kuniokoa. Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa kutoka kwa watesi wetu; Na watuchukiao umewaaibisha. Tumejisifia Mungu mchana kutwa, Na jina lako tutalishukuru milele.

Soma Zaburi 44