Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 3:1-8

Zaburi 3:1-8 SRUV

BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu, Waliojipanga Juu yangu pande zote. BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. Wokovu ni wa BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Soma Zaburi 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 3:1-8

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha