Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 27

27
Wimbo wa ushindi katika Bwana wa Daudi
Ya Daudi.
1BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
BWANA ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani?
2Watenda mabaya waliponikaribia,
Wanile nyama yangu,
Watesi wangu na adui zangu,
Walijikwaa wakaanguka.
3Jeshi lijapojipanga kupigana nami,
Moyo wangu hautaogopa.
Vita vijaponitokea,
Hata hapo nitatumainia BWANA.
4Neno moja nimelitaka kwa BWANA,
Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa BWANA
Siku zote za maisha yangu,
Niutazame uzuri wa BWANA,
Na kutafakari hekaluni mwake.
5 # Mit 18:10; Isa 4:6; Kol 3:3 Maana atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya,
Atanisitiri katika sitara ya hema yake,
Na kuniinua juu ya mwamba.
6Na sasa kichwa changu kitainuka
Juu ya adui zangu wanaonizunguka.
Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;
Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
7Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia,
Unifadhili, unijibu.
8Uliposema, “Nitafuteni uso wangu,”
Moyo wangu umekuambia,
BWANA, uso wako nitautafuta.
9Usinifiche uso wako,
Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira.
Umekuwa msaada wangu, usinitupe,
Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
10 # Isa 49:15; Yn 16:32; 2 Tim 4:16-18 Hata baba yangu na mama yangu wakiniacha,
Bali BWANA atanikaribisha kwake.
11Ee BWANA, unifundishe njia yako,
Na kuniongoza katika njia iliyonyoka;
Kwa sababu yao wanaoniotea;
12 # 1 Sam 22:9; Mt 26:59,60 Usinitie katika nia ya watesi wangu;
Maana mashahidi wa uongo wamenijia,
Nao watoao jeuri kama pumzi.
13 # Zab 112:7,8 Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA
Katika nchi ya walio hai.
14 # Zab 62:1,5; Isa 25:9; Hab 2:3 Umtumainie BWANA, uwe imara,
Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 27: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha