Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 2

2
Ahadi ya Mungu kwa mtiwa mafuta wake
1 # Mdo 4:25-26 Mbona mataifa yanafanya ghasia,
Na watu kuwaza mambo ya bure?
2 # Zab 45:7; Yn 1:41 Wafalme wa dunia wanajipanga,
Na wakuu wanafanya shauri pamoja,
Juu ya BWANA,
Na juu ya masihi#2:2 Au, mtiwa mafuta. wake,
3 # Lk 19:14 Na tuvipasue vifungo vyao,
Na kuzitupa mbali nasi kamba zao.
4 # Zab 11:4 Yeye aketiye mbinguni anacheka,
Bwana anawafanyia dhihaka.
5Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,
Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema:
6Nami nimemweka mfalme wangu
Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
7 # Mdo 13:33; Ebr 1:5; 5:5; Mt 8:29 Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,
Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
8 # Dan 7:13,14; Yn 17:4,5 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,
Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9 # Ufu 2:26-27; 12:5; 19:15; Mt 21:44 Utawaponda kwa fimbo ya chuma,
Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
10Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima,
Enyi watawala wa dunia, mwaonywa.
11Mtumikieni BWANA kwa kicho,
Shangilieni kwa kutetemeka.
12 # Yn 5:22,23; Yer 17:7 Shikeni yaliyo bora,#2:12 Au, Pokeeni mafundisho au, Mbu suni Mwana. asije akafanya hasira
Nanyi mkapotea njiani,
Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi;
Heri wote wanaomkimbilia.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha