Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 18:31-42

Zaburi 18:31-42 SRUV

Maana ni nani aliye Mungu ila BWANA? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Anaifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kulia umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezipanulia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza. Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala sitarudi nyuma hadi wakomeshwe. Nitawapigapiga wasiweze kusimama, Wataanguka chini ya miguu yangu. Nawe umenipa nguvu za vita, Hunitiishia chini yangu walionishambulia. Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Nao walionichukia nimewakatilia mbali. Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita BWANA lakini hakuwajibu, Nikawaponda kama mavumbi mbele ya upepo, Nikawatupa nje kama matope ya njiani.

Soma Zaburi 18