Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 146

146
Sifa kwa kupata msaada wa Mungu
1Haleluya.#146:1 Haleluya: maana yake ni, Msifuni BWANA.
Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.
2Nitamsifu BWANA muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
3 # Isa 2:22 Msiwatumainie wakuu,
Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4 # Mhu 12:7; 1 Kor 2:6 Pumzi yake inapomtoka, anarudi katika udongo wake,
Siku iyo hiyo mipango yake hutoweka.
5 # Yer 17:7 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,
6 # Mik 7:20; Mdo 4:24; 14:15; Ufu 14:7 Aliyezifanya mbingu na nchi,
Bahari na vitu vyote vilivyomo.
Huishika kweli milele,
7Huwafanyia hukumu walioonewa,
Huwapa wenye njaa chakula;
BWANA hufungua waliofungwa;
8BWANA huwafumbua macho waliopofuka;
BWANA huwainua walioinama;
BWANA huwapenda wenye haki;
9BWANA huwahifadhi wageni;
Huwategemeza yatima na mjane;
Bali njia ya wasio haki huiharibu.
10BWANA atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kwa vizazi vyote.
Haleluya.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 146: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia