Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 139:16-24

Zaburi 139:16-24 SRUV

Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Mawazo yako ni mazito sana kwangu; Ee Mungu; nayo ni makuu sana. Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga; Niamkapo ningali pamoja nawe. Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu; Wale wanaokusema kwa ubaya, na kutenda maovu juu ya jina lako bure. Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiudhike nao watu wanaokuasi? Nawachukia kwa upepo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu. Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Soma Zaburi 139

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 139:16-24