Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 139:16-24

Zab 139:16-24 SUV

Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo nikali pamoja nawe. Ee Mungu, laiti ungewafisha waovu! Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu; Kwa maana wakuasi kwa ubaya, Adui zako wakutaja jina lako bure. Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisikirihike nao wakuasio? Nawachukia kwa ukomo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu. Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Soma Zab 139

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 139:16-24