Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 126

126
Mavuno ya shangwe
Wimbo wa kupanda mlima.
1 # Mdo 12:9 BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.
2 # Ayu 8:21 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,
Na ulimi wetu kelele za furaha.
Ndipo waliposema katika mataifa,
BWANA amewatendea mambo makuu.
3BWANA alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi.
4Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa,
Kama vijito vya Kusini.
5 # Isa 12:1-3; Yer 31:9; Yoe 2:17; Mt 5:4; 2 Kor 7:8-11 Wapandao kwa machozi
Watavuna kwa kelele za furaha.
6Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 126: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia