Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 121:1-8

Zaburi 121:1-8 SRUV

Nayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia; Naam, hatasinzia wala hatalala, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Soma Zaburi 121

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 121:1-8

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha