Zaburi 119:5-8
Zaburi 119:5-8 SRUV
Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako. Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa.