Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 115:1-18

Zaburi 115:1-18 SRUV

Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi, Bali ulitukuze jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako, Kwa ajili ya uaminifu wako. Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao? Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda. Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazinusi harufu, Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazitengenezao watafanana nazo, Sawa na wote wanaozitumainia. Enyi Israeli, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao. Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao. Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao. BWANA ametukumbuka, Naye atatubariki sisi. Ataubariki mlango wa Israeli, Ataubariki mlango wa Haruni, Atawabariki wamchao BWANA, Wadogo kwa wakubwa. BWANA na awaongeze ninyi, Ninyi na watoto wenu. Na mbarikiwe ninyi na BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu. Wafu hawamsifu Mungu BWANA, Wala yeyote ashukaye kwenye kimya; Bali sisi tutamhimidi BWANA, Tangu leo na hata milele.

Soma Zaburi 115

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 115:1-18