Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 110

110
Hakikisho la ushindi kwa mteule wa Mungu
Ya Daudi. Zaburi.
1 # Zab 45:6; Mt 22:44; Mk 12:36; Lk 20:42-43; 1 Kor 15:25; Mdo 2:34-35; 1 Kor 15:25; Efe 1:20-22; Kol 3:1; Ebr 1:13; 8:1; 10:12-13 Neno la BWANA kwa Bwana wangu,
Uketi upande wangu wa kulia,
Hadi niwafanyapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.
2BWANA atainyosha toka Sayuni
Fimbo ya nguvu zako.
Uwe na enzi kati ya adui zako;
3 # Amu 5:2; Zab 96:9; Mdo 2:41 Watu wako watajitoa kwa hiari,
Siku ya uwezo wako;
Kwa uzuri wa utakatifu,
Tokea tumbo la asubuhi,
Unao umande wa ujana wako.
4 # Hes 23:19; Zek 6:13; Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21 BWANA ameapa,
Wala hataghairi,
Ndiwe kuhani hata milele,
Kwa mfano wa Melkizedeki.
5 # Zab 16:8; 2:5; Rum 2:5; Ufu 11:18 Bwana yu mkono wako wa kulia;
Atawaponda wafalme,
Siku ya ghadhabu yake.
6 # Hab 3:13 Atahukumu kati ya mataifa,
Ataijaza nchi mizoga;
Atawaponda wakuu katika nchi nyingi.
7 # Isa 61:1; Yn 3:34; Isa 53:12 Atakunywa maji ya mto njiani;
Kwa hiyo atakiinua kichwa chake kwa ushindi.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 110: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia