Zaburi 106:1-5
Zaburi 106:1-5 SRUV
Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA, Au kuzihubiri sifa zake zote? Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote. Ee BWANA, unikumbuke mimi, Kwa kibali ulicho nacho kwa watu wako. Unijie kwa wokovu wako, Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.