Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki ni mojawapo ya “maandiko ya hekima” (tazama Utangulizi wa Agano la Kale). Jina la kitabu hiki latoka katika kitabu chenyewe (1:1; 10:1; 25:1). Maana yake ni maneno machache ya kisanii yatumiwayo kwa mfano au fumbo ili kueleza maana pana na ndefu kwa ajili ya mafundisho. Kama ilivyo hapa kwetu, wenye hekima walitumia machache ya kisanaa yaliyo rahisi kukumbuka ili kuwafunza watu maisha bora. Wenye hekima wa Israeli walioandika na waliokusanya pamoja mithali walifuata misingi ya imani yao. Uchaji kwa Mungu (1:7) na sheria ya Mungu. Uhusiano, mawasiliano na urafiki vinatawaliwa na sheria ya Mungu.
Kitabu hiki ni mkusanyo wa mithali mbalimbali zilizoandikwa na Waisraeli na baadhi toka mataifa jirani ya Israeli. Mfalme Sulemani ni mwandishi mkuu na mkusanyaji wa mithali (1 Fal 4:32; Mit 10:1; 25:1). Baadhi ya mithali zake zimewekwa katika kitabu hiki (Mit 25:12; 2 Nya 29:1—31:21). Pia kuna maneno ya watu wengine wenye hekima (22:17), Aguri (30:1), Mfalme Lemueli, (31:1), na asiyejulikana jina lake (31:10).
Ujumbe wa Mithali umeandikwa kwa mtindo wa mashairi ya Kiebrania (3:6; 11:5; 16:16,27). Hekima inazungumzwa kana kwamba ni mtu. Ni mafundisho ya maisha mazuri na ya heri. Kumcha Mungu ndio chanzo cha maarifa (14:17; 9:10; 15:33). Mwenye hekima hana budi kuwa mtiifu (10:1), mnyenyekevu (11:2; 15:33), mwenye busara na mvumilivu (14:17; 18:13; 25:28); mwadilifu (10:11), mkweli na mwaminifu (10:10; 12:22); mwenye huruma (11:17), mkarimu (11:25; 15:19; 22:13) na mtenda haki (21:15).
Yaliyomo:
1. Thamani ya hekima, Sura 1—9
2. Mithali za Sulemani, Sura 10:1—22:16
3. Misemo ya wenye hekima, Sura 22:17—24:34
4. Mithali nyingine za Sulemani, Sura 25—29
5. Maneno ya Aguri, Sura 30
6. Maneno ya mama yake Lemueli na Mke mwema, Sura 31

Iliyochaguliwa sasa

Mithali UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha