Mithali 29:22-27
Mithali 29:22-27 SRUV
Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana. Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Mshiriki wa mwizi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.