Mithali 22:22-29
Mithali 22:22-29 SRUV
Usimnyang'anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako? Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako. Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.