Mithali 1:10-16
Mithali 1:10-16 SRUV
Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni. Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote kwa shirika. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.