Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 8

8
Taa saba
1 # Kut 25:31-40; 37:17-24 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Kut 40:25; Law 24:1,2; Zab 119:105; Isa 8:20; Mt 5:14; Yn 1:9; 8:12 Nena na Haruni, ukamwambie, Utakapoziweka taa, hizo taa saba zitatoa nuru hapo mbele ya kinara cha taa. 3Basi Haruni akafanya; akaziweka taa zake ili zitoe nuru hapo mbele ya kinara, kama BWANA alivyomwagiza Musa. 4#Kut 25:18,31,40 Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu kitako chake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
Kuwekwa wakfu na huduma ya Walawi
5Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 6#Zab 26:6; Isa 52:11; Ebr 7:26; 10:22 Watwae Walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kisha uwatakase. 7#Law 14:8,9 Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa. 8#Law 2:1 Kisha na watwae ng'ombe dume mmoja mchanga, na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, nawe utatwaa ng'ombe dume mchanga mwingine kuwa sadaka ya dhambi. 9#Kut 29:4; 40:12; Law 8:3 Nawe utawaleta Walawi mbele ya hema ya kukutania; nawe utauitisha mkutano wote wa wana wa Israeli; 10#Law 1:4 nawe utawaleta Walawi mbele za BWANA; kisha wana wa Israeli wataweka mikono yao juu ya Walawi; 11naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe watumishi wa BWANA. 12#Kut 29:10; Law 1:4; 8:14 Kisha Walawi wataweka mikono yao juu ya vichwa vya hao ng'ombe; nawe umtoe mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA, na huyo wa pili awe sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi. 13Kisha utawaweka Walawi mbele ya Haruni, na mbele ya wanawe na kuwasongeza kwa BWANA wawe sadaka ya kutikiswa. 14#Hes 3:45; 16:9; Mal 3:17 Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu. 15#Kut 29:24 Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wahudumu katika hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. 16#Hes 3:12,45 Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu. 17#Kut 13:2,12-15; Lk 2:23; Hes 3:13 Kwa kuwa wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli ni wangu, wa wanadamu na wa wanyama; siku hiyo niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri niliwatakasa kwa ajili yangu mwenyewe. 18Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote walio katika wana wa Israeli. 19#Hes 3:9; 18:2-6; 1:53; 16:46; 18:5 Nami nimempa Haruni hao Walawi wawe kipawa chake yeye na wanawe, kutoka kwa wana wa Israeli, ili wafanye kazi ya kutumikia wana wa Israeli katika hema ya kukutania, kisha wafanye upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli; ili kusiwe na maradhi kati ya wana wa Israeli, hapo wana wa Israeli watakapopakaribia mahali patakatifu. 20Basi Musa na Haruni, na mkutano wote wa wana wa Israeli, wakawafanyia Walawi mambo hayo; kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa kwa habari za hao Walawi, ndivyo wana wa Israeli walivyowafanyia. 21#Rum 15:16 Walawi wakajitakasa na dhambi, nao wakafua nguo zao; kisha Haruni akawasongeza mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa; Haruni akafanya kwa ajili yao ili kuwatakasa. 22#2 Nya 30:15; 31:2 Kisha baada ya hayo Walawi wakaingia ili wafanye kazi zao ndani ya hema ya kukutania mbele ya Haruni na mbele ya wanawe; kama BWANA alivyomwagiza Musa kuhusu hao Walawi, ndivyo walivyowafanyia.
23Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 24#Hes 4:3; 1 Nya 23:3; 24:27 Mambo yawapasayo hao Walawi ni haya; tangu waliopata umri wa miaka ishirini na mitano na zaidi wataingia ndani ili wahudumu katika hema ya kukutania; 25tena tangu waliopata umri wa miaka hamsini wasiendelee kuhudumu tena; 26#Hes 1:53; 1 Nya 23:28-32; 26:20-29; Eze 44:8,11 lakini watawasaidia na ndugu zao katika hema ya kukutania, kufanya kazi zao, lakini wasitumike katika huo utumishi tena. Ndivyo utakavyowafanyia Walawi katika mambo ya ulinzi wao.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 8: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia