Hesabu 31
31
Vita juu ya Midiani
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Hes 25:17; Kum 32:35,43; Zab 94:1; Mwa 15:15; 25:8; 35:29; Hes 27:13 Walipizie kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako. 3#Kum 32:35; Yer 50:28; Zab 94:1; Rum 12:19; Ebr 10:30 Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipizia kisasi BWANA, juu ya Midiani. 4Katika kila kabila mtatoa watu elfu moja, katika kabila zote za Israeli, nanyi mtawatuma waende vitani. 5Basi walitolewa katika maelfu ya Israeli, elfu moja ya kila kabila, wanaume elfu kumi na mbili walioandaliwa kwa vita. 6#Hes 10:9 Basi Musa akawatuma watu elfu wa kila kabila waende vitani, wao na Finehasi mwana wa Eleazari kuhani, waende vitani, na vile vyombo vya mahali patakatifu, na hizo tarumbeta za kupiga sauti za kugutusha mkononi mwake. 7#Kum 20:13; Amu 21:11; 1 Sam 27:9; 1 Fal 11:15,16; Amu 6:1,2,33 Nao wakapigana na Midiani kama BWANA alivyomwagiza Musa; nao wakawaua kila mwanamume. 8#Yos 13:21; Hes 22:10; 24:25; Yos 13:22; Zab 9:12; Yud 1:11; Ufu 2:14; 19:20 Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga. 9Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara. 10Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na kambi yao yote wakayateketeza kwa moto. 11#Kum 20:14 Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama. 12Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo kambini katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
Kurejea toka Vitani
13Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya kambi. 14Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, hao waliorudi kutoka kupigana vita. 15#Kum 2:34; 20:13; Yos 6:21; 8:25; 10:40; 11:14; 1 Sam 15:3 Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai? 16#Hes 25:1-9; 24:14; Yos 22:17; Zab 106:28,29; Hos 9:10; Mik 6:5; 2 Pet 2:15; Ufu 2:14 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie BWANA dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hiyo pigo lilikuwa katika mkutano wa BWANA. 17#Amu 21:11 Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mwanamume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mwanamume kwa kulala pamoja naye. 18Lakini hao wasichana wote ambao hawakumjua mwanamume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa ajili yenu. 19#Hes 5:2; 19:11; 9:6,10 Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya kambi muda wa siku saba; mtu yeyote aliyemwua mtu, na yeyote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu. 20Na kuhusu kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe; 21Kisha Eleazari kuhani akawaambia wanaume wa vita wote waliokwenda vitani, Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyomwagiza Musa; 22lakini dhahabu, na fedha, na shaba, na chuma, na bati, na risasi, 23#Hes 8:7; 19:9,17 kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya utakaso; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji. 24#Law 11:25; 14:9; Hes 19:10,22; Zab 51:2; Zek 13:1; Efe 5:26; Ebr 9:9,10; 10:22; 1 Yoh 1:7 Nanyi mtazifua nguo zenu siku ya saba, nanyi mtakuwa safi, kisha baadaye mtaingia kambini.
Mgawanyo wa mateka na nyara
25Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 26Fanya jumla ya hayo mateka ya wanadamu, na ya wanyama pia, wewe, na Eleazari kuhani, na wakuu wa nyumba za baba za mkutano; 27#Yos 22:8; 1 Sam 30:4; Zab 68:12 ukagawanye nyara katika mafungu mawili; kati ya wanajeshi waliotoka nje kupigana vita na hio jumuiya nzima; 28#2 Sam 8:11; 1 Nya 18:11; 26:27; Isa 18:7; 23:18; Mt 22:21; Hes 18:26 kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya BWANA; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo; 29twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA. 30#Hes 3:7,8; 18:3,4; 1 Nya 9:27-29; 23:32 Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao wenye wajibu wa kuhudumu maskani ya BWANA. 31Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa. 32Basi masazo ya hizo nyara walizotwaa watu wa vita, zilikuwa ni kondoo elfu mia sita na sabini na tano, 33na ng'ombe elfu sabini na mbili, 34na punda elfu sitini na moja, 35tena wanadamu jumla yao ilikuwa elfu thelathini na mbili, katika hao wanawake ambao hawakumjua mwanamume kwa kulala pamoja naye. 36Na hiyo nusu ambayo ilikuwa ni sehemu ya hao waliotoka kwenda vitani, idadi yake ilikuwa kondoo elfu mia tatu na thelathini na saba na mia tano; 37#Law 25:23; Kum 10:14; Zab 24:1; 50:12; Mit 3:9; Mt 22:21; Mk 12:17; Lk 20:25; 1 Kor 10:26,28 na kodi ya BWANA katika hao kondoo ilikuwa kondoo mia sita na sabini na watano. 38Tena, ng'ombe walikuwa elfu thelathini na sita; na katika hao kodi ya BWANA ilikuwa ng'ombe sabini na wawili. 39Na punda walikuwa elfu thelathini na mia tano, katika hao kodi ya BWANA ilikuwa punda sitini na mmoja. 40Na wanadamu walikuwa watu elfu kumi na sita; katika hao sehemu ya BWANA ilikuwa ni watu thelathini na wawili. 41#Hes 5:9,10; 18:8,19 Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa. 42Tena katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, ambayo Musa aliitenga na watu waliokwenda vitani, 43(basi hiyo nusu ya mkutano ilikuwa ni kondoo elfu mia tatu na thelathini na saba na mia tano, 44na ng'ombe elfu thelathini na sita, 45na punda elfu thelathini, na mia tano, 46na wanadamu elfu kumi na sita;) 47na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, wenye wajibu wa kuhudumu katika maskani ya BWANA; kama BWANA alivyomwagiza Musa. 48Na majemadari waliokuwa juu ya maelfu ya hilo jeshi, na viongozi wa maelfu, na viongozi wa mamia, wakamkaribia Musa; 49#Kut 23:7; Law 26:7-9; Zab 72:14; 116:15; 1 Sam 30:19 wakamwambia Musa wakisema, Sisi watumishi wako tumefanya jumla ya hesabu ya watu wa vita walio chini ya mikono yetu, na hapana hata mmoja aliyetupungukia. 50#Kut 30:12,16; Law 17:11; Mt 20:28; Rum 3:25 Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za mhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA. 51Musa na Eleazari kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa. 52Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa BWANA, ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, ilikuwa shekeli elfu kumi na sita, mia saba na hamsini. 53#Kum 20:14 (Kwa kuwa wanajeshi walikuwa wamechukua nyara kila mtu zake binafsi.) 54#Hes 16:40; Kut 30:16; Yos 4:7; Zek 6:14; Lk 22:19; Mdo 10:4 Basi Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao makamanda wa maelfu na wa mamia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za BWANA.
Iliyochaguliwa sasa
Hesabu 31: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.