Hesabu 25
25
Ibada ya Baali na Peori
1 #
Hes 33:49; Mik 6:5; Hes 31:16; Ufu 2:14 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2#Yos 22:17; Hos 9:10; Kut 34:15; 20:5 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3#Zab 106:29 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za BWANA zikawaka juu ya Israeli. 4#Yos 22:17; Kum 13:17 Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa watu hao, uwanyongee juani mbele ya BWANA ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli. 5#Kut 32:27; 1 Fal 18:40 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. 6#Yoe 2:17 Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 7#Kut 6:25 Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; 8akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. 9#1 Kor 10:8 Nao waliokufa kwa pigo hilo idadi yao ilikuwa elfu ishirini na nne.
10Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, 11#Zab 106:30; Kut 20:5; Zab 78:53; Nah 1:2; Sef 1:13 Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. 12#Mal 3:1 Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; 13#1 Nya 6:4; Kut 40:15; Mdo 22:3 tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli. 14Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni. 15Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani.
16Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 17Wasumbue Wamidiani, na kuwapiga; 18kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, dada yao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori.
Iliyochaguliwa sasa
Hesabu 25: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.