Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 14

14
Watu wanaasi
1Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. 2#Zab 106:25; Kum 28:68 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? 4#Neh 9:17; Mdo 7:39; Ebr 11:15 Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe kiongozi, tukarudi Misri. 5Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko la wana wa Israeli. 6Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; 7wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. 8#Kum 10:15; 2 Sam 15:25; 1 Fal 10:9; Zab 22:8; Isa 62:4; Hes 13:27 Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. 9#Ebr 3:16; Kum 9:7,23,24; Kum 20:3; Hes 24:8; Mwa 48:21; Kut 33:16; Kum 20:1; 2 Nya 15:2; Isa 41:10 Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope. 10#Kut 17:4; 16:10; Law 9:23 Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.
11 # Ebr 3:8; Zab 78:22; Yn 12:37 BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hadi lini? Wasiniamini hadi lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao. 12#Kut 32:10 Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.
Musa awaombea watu kwa Mungu
13 # Kut 32:11-14; Eze 20:9 Basi Musa akamwambia BWANA, Ndipo Wamisri watasikia habari hiyo; kwa kuwa wewe uliwaleta watu hawa kwa uweza wako, kutoka kati yao; 14#Kut 15:14; Neh 9:12 kisha watawaambia wenyeji wa nchi hii; wamesikia wao ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa; maana, wewe BWANA waonekana uso kwa uso, na wingu lako lasimama juu yao, kisha wewe watangulia mbele yao, katika nguzo ya wingu mchana, na katika nguzo ya moto usiku. 15Basi kama wewe ukiwaua watu hawa mfano wa mtu mmoja, ndipo mataifa yaliyosikia habari za sifa zako watakaponena na kusema, 16#Yos 7:9 Ni kwa sababu yeye BWANA hakuweza kuwaleta watu hao kuwatia katika nchi aliyowaapia, kwa ajili ya hayo amewaua nyikani. 17Basi sasa nakusihi sana, uweza wa Bwana wangu na uwe mkuu, kama ulivyonena, uliposema, 18#Kut 20:5-6; 34:6-7; Kum 5:9-10; 7:9-10; Zab 103:8; 145:8; Yon 4:2; Kut 34:7 BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yoyote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne. 19Nakusihi, usamehe uovu wa watu hawa, kama ukuu wa rehema yako ulivyo, kama ulivyowasamehe watu hawa, tangu huko Misri hata hivi sasa. 20#Yak 5:16; 1 Yoh 5:14 BWANA akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa; 21#Ebr 3:18; Zab 72:19; Isa 5:16; 11:9; 61:11; Eze 18:3; Hab 2:14; Ufu 11:15 lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA; 22#Kum 1:31,34; Zab 95:11; Ebr 4:6,7; Mwa 31:7 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu; 23#Kum 1:35; Zab 106:26; Eze 20:15; Ebr 3:18; 4:3 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona; 24#Yos 14:9-12; Zab 25:13; Isa 33:15; Mt 5:5 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye amenifuata kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na wazao wake wataimiliki. 25Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu.#14:25 Au Bahari ya Mafunjo.
Ukaidi wa Waisraeli na kushindwa kwao
26Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 27#Kut 16:28; Mt 17:17; Mk 9:19; Kut 16:12; 1 Kor 10:10 Je! Nivumilie na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hadi lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo. 28#Ebr 3:17 Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi; 29#Hes 26:64 mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia, 30#Kum 1:36,38 hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliapa kwa kuinua mkono wangu, kwamba nitawafanyia makao humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. 31#Zab 106:24; Mit 1:25,26; Ebr 12:16,17 Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi mliyoikataa ninyi. 32#1 Kor 10:5 Lakini katika habari zenu, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili. 33#Mdo 7:36; Zab 107:40; Kum 2:14 Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arubaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hadi maiti zenu zitakapoangamia jangwani. 34#Hes 13:25; Zab 95:10; Eze 4:6; 1 Fal 8:56; Zab 77:8; Ebr 4:1 Kwa jumla ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arubaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arubaini, nanyi mtakujua kuchukizwa kwangu. 35#Hes 23:19 Mimi BWANA nimekwisha nena, hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote, waliokusanyika juu yangu; wataangamia katika nyika hii, nako ndiko watakakokufa. 36#Hes 13:31 Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung'unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi, 37#Yer 28:16,17; 1 Kor 10:10; Ebr 3:17; Yud 1:5 watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA. 38#Yos 14:6 Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.
39 # Mit 19:3; Mt 8:12; Ebr 12:17 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaomboleza sana. 40#Kum 1:41; Mhu 9:3; Mt 7:21; Lk 13:25 Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi. 41#2 Nya 24:20; Ayu 9:4; Isa 59:1,2; Yer 2:37; 1 Kor 10:22 Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyakaidi maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo. 42#Kum 1:42; Zab 44:1-3 Msikwee, kwa kuwa BWANA hayumo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu. 43#Kum 1:43,44; Amu 16:20 Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimfuate BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi. 44Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la Agano la BWANA halikutoka humo kambini, wala Musa hakutoka. 45Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakateremka, wakawapiga na kuwaangusha, hadi wakafika Horma.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 14: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

Videos for Hesabu 14