Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nehemia 13

13
Wageni watengwa kutoka Israeli
1 # Kum 23:3; Amo 2:1-3 Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele; 2#Hes 22:5; Yos 24:9; Hes 23:8-11; Kum 23:5; Zab 109:28; Mik 6:5 kwa sababu hawakuwalaki wana wa Israeli kwa chakula na maji, bali walimwajiri Balaamu juu yao ili awalaani; lakini Mungu aliigeuza ile laana kuwa baraka. 3#Neh 9:2; Yak 1:27 Ikawa walipoisikia Torati, wakawatenga Israeli na umati wa watu waliochanganyika nao.
Matengenezo ya Nehemia
4Na kabla ya hayo, Eliashibu, kuhani, aliyewekwa avisimamie vyumba vya nyumba ya Mungu wetu, kwa kuwa alikuwa jamaa yake Tobia, 5alikuwa amemtengenezea chumba kikubwa, hapo walipoweka zamani sadaka za unga, na ubani, na vyombo, na zaka za nafaka, na divai, na mafuta, walivyoamriwa kuwapa Walawi, na waimbaji, na mabawabu; tena sadaka za kuinuliwa zilizokuwa za makuhani. 6#Neh 5:14 Lakini wakati huo wote mimi sikuwako huko Yerusalemu; maana katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta, mfalme wa Babeli, nilimrudia mfalme; na baada ya siku kadhaa nikaomba ruhusa tena kwa mfalme. 7Nami nikaja Yerusalemu, nikafahamu yale mabaya, ambayo Eliashibu ameyatenda kwa ajili ya Tobia, kwa kumtengenezea chumba katika nyua za nyumba ya Mungu. 8#Zab 69:9; Mk 11:15-17; Yn 2:13 Nami nikasikitika sana; basi nikavitupa nje vyombo vyote vya Tobia vitoke humo chumbani. 9#2 Nya 29:5 Kisha nikatoa amri, nao wakavisafisha vyumba; nami nikavirudisha humo vyombo vya nyumba ya Mungu, pamoja na sadaka za unga na ubani.
10 # Neh 10:37; Mal 3:8; 1 Tim 5:17,18; Hes 35:2 Tena nikagundua kwamba Walawi hawakupewa sehemu zao; Hivyo Walawi na waimbaji walioongoza ibada, kila mtu amerudi shambani mwake. 11#Mit 28:4; 1 Sam 2:17 Ndipo nikagombana na viongozi, nikasema, Mbona nyumba ya Mungu imeachwa? Kisha nikawakusanya, nikawaweka mahali pao. 12#Neh 12:44 Ndipo Yuda wote walipoleta zaka za nafaka, na mvinyo, na mafuta, kwenye hazina. 13#1 Kor 4:2 Nami nikawaweka watunza hazina juu ya hazina, yaani, Shelemia kuhani, na Sadoki mwandishi, na wa Walawi, Pedaya; na wa pili wao alikuwa Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania; kwani walihesabiwa kuwa waaminifu, na ilikuwa juu yao kuwagawia ndugu zao. 14#Neh 5:19 Unikumbukie hayo, Ee Mungu wangu, wala usifute fadhili zangu nilizozitenda kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, na kwa taratibu zake.
Matengenezo ya Sabato
15 # Kut 20:10; Yer 17:21 Siku hizo niliona katika Yuda watu wengine waliosindika zabibu ili kupata mvinyo siku ya sabato, na wengine waliochukua miganda, na kuwapakia punda zao; tena na mvinyo, na zabibu, na tini, na namna zote za mizigo, waliyoileta Yerusalemu, siku ya sabato; nami nikashuhudia juu yao siku ile waliyouza vyakula. 16Tena watu wa Tiro walioleta samaki na biashara za kila namna wakakaa mumo humo, wakawauzia watu wa Yuda na Yerusalemu siku ya sabato. 17Ndipo nikagombana na wakuu wa Yuda, nikawaambia, Ni neno baya gani hili mnalofanya ninyi, na kuinajisi siku ya sabato? 18Je! Sivyo hivyo walivyofanya baba zenu; na Mungu wetu, je! Hakuyaleta mabaya haya yote juu yetu, na juu ya mji huu? Nanyi hata hivyo mnazidi kuleta ghadhabu juu ya Israeli kwa kuinajisi sabato! 19#Law 23:32; Kut 31:14-17; Neh 7:3 Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, niliamuru milango ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wowote siku ya sabato. 20Basi wenye biashara na wachuuzi wa bidhaa za kila namna wakalala nje ya Yerusalemu mara moja au mbili. 21Ndipo nikawashuhudia, nikawaambia, Mbona mnalala nje ya mji? Mkitenda hivi tena, nitawakamata. Tangu wakati ule hawakuja tena siku ya sabato. 22#Neh 12:30 Kisha nikawaamuru Walawi wajitakase, nao waje kuyalinda malango, ili kuitakasa siku ya sabato. Unikumbukie hayo nayo, Ee Mungu wangu, ukaniachilie sawasawa na wingi wa rehema zako.
Ndoa za mseto zapigwa marufuku
23Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu; 24na nusu ya watoto wao wakazungumza kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kuzungumza Kiyahudi, bali kwa lugha mojawapo ya watu hao. 25#Mit 28:4; Kum 25:2; Ezr 7:26; 10:5; Neh 10:29,30 Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. 26#1 Fal 11:1; 2 Sam 12:24,25 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye. 27#Ezr 10:2 Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumkosea Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni? 28#Neh 12:10 Na mwana mmoja wa Yoyada, mwana wa Eliashibu, kuhani mkuu, alikuwa mkwewe Sanbalati, Mhoroni, basi nikamfukuza kwangu. 29#Neh 6:14; Mal 2:4 Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, jinsi walivyounajisi ukuhani, na agano la ukuhani na la Walawi. 30#Neh 10:30; 12:1 Hivyo nikawatakasa na kila kitu kigeni, nami nikawawekea zamu makuhani na Walawi, kila mtu kazini mwake; 31na kuleta kwa kuni na malimbuko, katika nyakati zilizoamriwa. Nikumbuke, Ee Mungu wangu, ili unitendee mema.

Iliyochaguliwa sasa

Nehemia 13: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha