Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nehemia 1

1
Nehemia awaombea watu wake
1 # Neh 10:1; Ezr 7:8; Neh 2:1; Est 1:2; Dan 8:2 Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kislevu,#1:1 Katika kalenda ya Kiyahudi Kislevu ni mwezi wa tisa. mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni, 2Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliosalimika, ambao hawakuchukuliwa uhamishoni na habari za Yerusalemu. 3#Neh 2:17; Isa 5:5; Yer 5:10; 2 Fal 25:10 Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto. 4Hapo niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadhaa; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni; 5#Kum 10:17; Neh 4:14; Ayu 37:22; Kut 20:6; Kum 7:9; Zab 89:2; Ebr 6:13-18 nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake; 6#1 Fal 8:28,29; 2 Nya 6:40; Dan 9:20 tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi. 7#Zab 106:6; Kum 28:15 Tumetenda maovu mengi juu yako, wala hatukuzishika amri, wala sheria, wala hukumu, ulizomwamuru Musa, mtumishi wako. 8#Law 26:33; Kum 4:25 Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa; 9#Law 26:39; Kum 4:29; 30:4 bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo. 10#Kum 9:29; Dan 9:15 Basi watu hao ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa uweza wako mwingi, na kwa mkono wako hodari. 11#Zab 119:4; Isa 26:8; Ebr 13:18; Mwa 32:11; Zab 37:5; Mit 16:3 Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nilikuwa mnyweshaji wa mfalme).

Iliyochaguliwa sasa

Nehemia 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha