Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 4:1-11

Mathayo 4:1-11 SRUV

Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ikiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Soma Mathayo 4

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 4:1-11