Mathayo 3:1-3
Mathayo 3:1-3 SRUV
Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Yudea, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.