Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 8:40-48

Luka 8:40-48 SRUV

Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana wote walikuwa wakimngojea. Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake; kwa kuwa binti yake yu karibu kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga. Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu yeyote, alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka. Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara moja. Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya; nenda zako na amani.

Soma Luka 8

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 8:40-48

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha