Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 24:45-53

Luka 24:45-53 SRUV

Ndipo akawafunua akili zao wapate kuelewa maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hadi mvikwe uwezo utokao juu. Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kuu. Nao daima walikuwa ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.

Soma Luka 24

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 24:45-53