Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 27

27
Sadaka za kuwekwa wakfu
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Mwa 28:20-22; Hes 6:2; Kum 23:21-23; Amu 11:30-39; 1 Sam 1:11,28; Ayu 22:27; Yon 1:16; Mdo 21:23 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtu atakapoondoa nadhiri, hizo nafsi za watu zitakuwa kwa BWANA, kama utakavyowahesabia wewe. 3#Kut 30:13; Hes 3:47; 18:16; Eze 45:12 Na hesabu yako itakuwa kwa mwanamume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu. 4Kama ni mwanamke, hesabu yako itakuwa shekeli thelathini. 5Tena akiwa na umri wa miaka mitano hata umri wa miaka ishirini, ndipo hesabu yako itakuwa shekeli ishirini kwa mwanamume, na shekeli kumi kwa mwanamke. 6Tena akiwa na umri wa mwezi mmoja hadi miaka mitano, ndipo hesabu yako itakuwa shekeli tano za fedha kwa mwanamume na shekeli tatu za fedha kwa mwanamke. 7Tena akiwa na umri wa miaka sitini na kuzidi; kama ni mwanamume, hesabu yako itakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke shekeli kumi. 8#Law 12:8; 14:21,22; Lk 21:1; 2 Kor 8:12 Lakini akiwa ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamkadiria; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomkadiria.
9Tena kama ni mnyama wa namna ambayo watu husongeza kuwa sadaka kwa BWANA, kila mmoja katika wanyama hao atakayetolewa kwa BWANA, na mtu yeyote, atakuwa ni mtakatifu. 10Yeye hatamgeuza, wala kumbadili mwema kwa mbaya, au mbaya kwa mwema; ikiwa atabadili mnyama kwa mnyama yeyote, ndipo mnyama huyo na yule waliobadiliwa wote wawili watakuwa watakatifu. 11Na kama ni mnyama yeyote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa BWANA, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani; 12na kuhani atamkadiria, akiwa mwema akiwa mbaya; kama kuhani atakavyomkadiria, ndivyo itakavyokuwa. 13Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako. 14#Law 25:29-31; Hes 18:14; 2 Kor 9:10 Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa. 15Tena mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali yake.
16Tena kama mtu akiweka wakfu kwa BWANA sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha. 17Ikiwa anaweka shamba lake liwe wakfu tangu mwaka wa jubilii, litakadiriwa vivyo hivyo kama hesabu yako ilivyo. 18#Law 25:15,16 Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya jubilii, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa jubilii, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa. 19Na kama yeye aliyeliweka shamba wakfu akitaka kulikomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nalo litathibitishwa kwake. 20Lakini asipotaka kulikomboa shamba, au kama amemwuzia mtu mwingine hilo shamba, halitakombolewa tena kabisa; 21#Law 25:10,28,31; Hes 18:14; Eze 44:29 ila hilo shamba litakuwa takatifu kwa BWANA litakapotoka katika jubilii, kama ni shamba lililowekwa wakfu; litakuwa mali ya kuhani. 22Tena kama akiweka wakfu kwa BWANA shamba ambalo amelinunua, ambalo si shamba la milki yake; 23ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa jubilii: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa BWANA. 24#Law 25:28 Mwaka wa jubilii shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake. 25#Kut 30:13; Hes 3:47; 18:16; Eze 45:12 Na hesabu zako zote zitaandamana shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini zitakuwa shekeli moja.
26 # Kut 13:2,12; 22:30; Hes 18:17; Kum 15:19 Mzaliwa wa kwanza tu katika wanyama, aliyewekwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa BWANA, mtu yeyote hatamweka kuwa mtakatifu; kama ni ng'ombe, kama ni kondoo, huyo ni wa BWANA. 27Na kama ni wa mnyama asiye safi, ndipo atamkomboa kama hesabu yako ilivyo, naye ataongeza sehemu ya tano ya bei yake; au asipokombolewa, ndipo atauzwa kama hesabu yako ilivyo.
28 # Hes 18:14; Yos 6:17; Amu 11:30,31 Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu chochote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa BWANA, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa BWANA. 29Kila aliyewekwa wakfu, aliyewekwa wakfu na binadamu, hatakombolewa; sharti atauawa.
30 # Hes 18:21; Kum 14:22-29; Mwa 28:22; 2 Nya 31:5; Neh 13:12 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA. 31Na kama mtu akitaka kukomboa chochote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake. 32#Yer 33:13; Eze 20:37; Mik 7:14 Tena zaka yote ya ng'ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA. 33Hataangalia kama ni mwema au ni mbaya, wala hatambadili; na kama akimbadili na yoyote, ndipo wote wawili, huyo na huyo waliobadiliwa watakuwa ni watakatifu; hatakombolewa.
34Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 27: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

Videos for Mambo ya Walawi 27