Yoshua 9
9
Wagibeoni wajiokoa kwa hila
1 #
Hes 34:6; Mwa 15:18,21; Kut 3:17; 23:23; Kum 7:1 Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo; 2#1 Nya 20:1; Zab 2:1,2; 83:3,5; Mit 11:21; Isa 8:9-12; Yoe 3:9-12; Mdo 4:26-28 ndipo walipojikutanisha pamoja wenyewe kwa wenyewe, ili kupigana na Yoshua, na hao Israeli, kwa nia moja.
3 #
Yos 10:2; 2 Sam 21:1,2; Yos 6:27 Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai, 4#Ayu 32:19; Mt 9:17; Lk 5:37,38 wao wakatenda kwa hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyorarukararuka, na kutiwa viraka; 5na viatu vilivyotoboka na kushonwashonwa katika miguu yao, na mavazi makuukuu tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa umekauka na kuota ukungu. 6#Yos 5:10 Nao wakamwendea Yoshua hadi kambini huko Gilgali, nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi. 7#Kut 23:32; 34:12; Kum 7:2; Yos 11:19; Amu 2:2 Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mnakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi? 8#Kum 20:11; 2 Fal 10:5 Nao wakamwambia Yoshua, Sisi tu watumishi wako. Yoshua akawauliza, Ninyi ni nani? Na mnatoka wapi? 9#Kum 20:15; Kut 15:14; Yos 2:10 Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako tunatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la BWANA, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri, 10#Hes 21:21-35 na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi. 11Kisha wazee wetu, na wenyeji wote wa nchi yetu, walinena nasi na kutuambia, Chukueni vyakula mkononi mwenu kwa ajili ya safari, mwende mkawalaki watu hao, na kuwaambia, Sisi tu watumishi wenu; basi sasa fanyeni agano nasi. 12Huu mkate wetu tuliutwaa ukiwa bado moto katika nyumba zetu, siku hiyo tuliyotoka kuja kwenu, uwe chakula chetu; lakini sasa, tazama, umekauka, na kuingia ukungu; 13na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa ni vipya; sasa, tazama, vimerarukararuka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana. 14#Hes 27:21; Amu 1:1; 1 Sam 22:10; 23:10,11; 30:8; 2 Sam 2:1; 5:19; Isa 30:1,2 Basi wakuu hao#9:14 au watu hao. wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa BWANA. 15#2 Sam 21:2 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia. 16Kisha ikawa, mwisho wa siku ya tatu baada ya kufanya hilo agano nao, walisikia habari ya kuwa watu hao ni jirani zao, na ya kwamba waliketi kati yao. 17#Yos 18:25; Ezr 2:25 Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu.
18 #
Zab 15:4
Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu. 19Lakini wakuu wote waliwaambia mkutano wote, Sisi tumewaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli; basi sasa hatuwezi kuwagusa watu hawa. 20#2 Sam 21:1; Eze 17:13-18; Zek 5:3,4; Mal 3:5 Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho kiapo tulichowaapia. 21#Kum 29:11 Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia. 22Basi Yoshua akawaita, akanena nao, na kuwaambia, Mbona ninyi mmetudanganya, huku mkisema, Sisi tu mbali sana na ninyi; nanyi kumbe! Mnakaa kati yetu? 23#Mwa 9:25 Basi sasa mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu. 24#Kut 23:32; Hes 33:51-56; Kum 7:1,2; 20:15-17; Kut 15:14 Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo BWANA, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili. 25#Mwa 16:6 Basi sasa, tazama, sisi tu mkononi mwako; basi kama uonavyo kuwa ni vyema na haki kwako wewe kututenda, tutende hivyo. 26Naye akawafanyia hivyo, na kuwaokoa na mkono wa wana wa Israeli, ili wasiwaue. 27#Kum 12:5; 1 Fal 8:29; 9:7; 2 Nya 7:12,20; Zab 78:68 Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya BWANA, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.
Iliyochaguliwa sasa
Yoshua 9: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.