Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 24

24
Makabila wafanya agano upya
1 # Mwa 12:6; 33:18,19; Amu 9:1-3; 1 Fal 12:1; Kut 18:25; Yos 23:2; 1 Sam 10:10; Mdo 10:33 Yoshua akawakusanya makabila yote ya Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maofisa wao nao wakaja mbele za Mungu. 2#Mwa 11:26,27; 12:1; Kum 26:5; Isa 51:2; Mwa 31:53 Yoshua akawaambia watu wote, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Abrahamu na Nahori; waliitumikia miungu mingine. 3#Mwa 12:1-9; 21:1-3; Mdo 7:2,3; Zab 127:3 Nami nikamtwaa Abrahamu baba yenu toka ng'ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka. 4#Mwa 25:24-26; 36:8; 46:1-7; Kum 2:5; Mdo 17:26 Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri. 5#Kut 3:10; 7:1—12:42 Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi. 6#Kut 14:1-31; Kut 12:37,51; Mik 6:4; Neh 9:11; Zab 77:15-20; 78:13; Isa 63:12,13; Mdo 7:36; Ebr 11:29 Nikawatoa baba zenu watoke Misri; nanyi mkaifikia bahari; Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka Bahari ya Shamu. 7Nao walipomlilia BWANA, akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi. 8#Hes 21:21-35; Kum 2:32; 3:1 Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani; nao wakapigana nanyi; nikawatia mikononi mwenu, mkaimiliki nchi yao; nami nikawaangamiza mbele yenu. 9#Amu 11:25; Hes 22:5 Ndipo Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, akainuka, akapigana na Israeli; tena akatuma watu kumwita Balaamu, mwana wa Beori, aje awalaani; 10#Kum 23:5; Hes 23:11 lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu; kwa hiyo akafululiza kuwabariki; basi nikawatoa katika mkono wake. 11#Yos 4:14-17; 6:1-21 Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu. 12#Kut 23:28; Kum 7:20; Zab 44:3,6 Nikatuma nyigu mbele yenu, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako. 13#Kum 6:10-11; 8:7; Yos 11:13; Mit 13:22 Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.
14 # Kum 10:12; 1 Sam 12:24; Ayu 1:1; Mdo 9:31; Mwa 17:1; 20:5; Kum 18:13; Zab 119:1; 2 Kor 1:12; Efe 6:24; Law 17:7; Eze 20:7 Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA. 15#Kut 23:24; Kum 13:7; Amu 6:10; Mwa 18:19 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. 16Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache BWANA, ili kuitumikia miungu mingine; 17kwa maana BWANA, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao. 18BWANA ndiye aliyewafukuza watu wa mataifa yote watoke mbele yetu, naam, Waamori waliokaa katika nchi hii; basi, kwa sababu hiyo sisi nasi tutamtumikia BWANA, maana yeye ndiye Mungu wetu. 19#Rut 1:15; Mt 6:24; Lk 14:25-33; Law 19:2; 1 Sam 6:20; Zab 99:5,9; Isa 5:16; Kut 23:21; Isa 27:11 Yoshua akawaambia watu, Hamwezi kumtumikia BWANA; kwa kuwa yeye ni Mungu mtakatifu; yeye ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa yenu, wala dhambi zenu. 20#Yos 23:12-15; 2 Nya 15:2; Ezr 8:22; Isa 1:28; 63:10; Yer 17:13; Ebr 10:26-28; Mdo 7:42 Kama mkimwacha BWANA na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema. 21Lakini hao watu wakamwambia Yoshua, La! Lakini tutamtumikia BWANA. 22#Zab 119:173 Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua BWANA, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi. 23#Mwa 35:2; 1 Sam 7:3 Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. 24Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii. 25#Kut 15:25; 2 Fal 11:17 Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.
26 # Kum 31:24; Amu 9:6; Mwa 28:18; Yos 4:3 Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha Torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa BWANA. 27#Mwa 31:48; Kum 31:19; 32:1 Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya BWANA aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu. 28Basi Yoshua akawaruhusu watu, wakaenda zao, kila mtu kwenye urithi wake.
Kifo cha Yoshua na Eleazari
29Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, mwenye umri wa miaka mia moja na kumi. 30#Yos 19:49-50; Amu 2:9 Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-sera; ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi. 31#Amu 2:7 Nao Israeli wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya BWANA, aliyowatendea Israeli.
32 # Mwa 33:19; 50:24-25; Kut 13:19; Yn 4:5; Mdo 7:16 Na hiyo mifupa ya Yusufu, ambayo wana wa Israeli walikuwa wameileta kutoka Misri, wakaizika huko Shekemu katika ile sehemu ya nchi, Yakobo aliyoinunua kwa wana wa Hamori, babaye Shekemu, kwa vipande mia moja vya fedha; nayo ikawa ni urithi wa wana wa Yusufu. 33#Kut 6:25; Amu 20:28 Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.

Iliyochaguliwa sasa

Yoshua 24: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia