Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 22

22
Makabila ya mashariki warudi katika nchi zao
1Wakati huo Yoshua akawaita Wareubeni, na Wagadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, 2#Hes 32:20-32; Yos 1:12-15,16,17; Kum 3:18 naye akawaambia, Ninyi mmeyafuata hayo yote mliyoamriwa na Musa, mtumishi wa BWANA, nanyi mmeisikia sauti yangu katika yote niliyowaamuru mimi; 3hamkuwaacha hao ndugu zenu siku hizi nyingi hata hivi leo, lakini mmeyashika maagizo ya amri ya BWANA, Mungu wenu. 4#Hes 32:33; Kum 29:8; Yos 13:8 Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani. 5#Kum 6:6,17; 11:22; 2 Fal 10:31; Zab 119:4; Mt 22:36; Rum 13:10; 1 Tim 1:5; Kum 10:12; Yos 23:11; Lk 11:42; Yn 15:9,10; 1 Yoh 5:3; 2 Yoh 1:6; Yud 1:21 Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote. 6#Mwa 47:7; Kut 39:43; Yos 14:13; 2 Sam 6:18; Lk 24:50 Basi Yoshua akawabariki, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao.
7 # Yos 17:5 Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila la Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowaruhusu waende zao mahemani kwao, akawabariki, 8#Hes 31:27; 1 Sam 30:14 kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng'ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavazi mengi sana; mgawane na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu.
9 # Hes 32:26,29 Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.
Madhabahu ya ukumbusho
10Nao walipofika pande za Yordani#22:10 Au ‘Gelilothi ya Yordani’. zilizo katika nchi ya Kanaani, hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na nusu ya kabila la Manase, wakajenga madhabahu huko karibu na Yordani, iliyoonekana kuwa ni madhabahu kubwa. 11#Law 17:8; Kum 13:12; Amu 20:12 Wana wa Israeli walisikia ikinenwa, Tazama, wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamejenga madhabahu huko upande wa mbele wa nchi ya Kanaani, katika nchi#22:11 Au Gelilothi iliyo karibu na Yordani. iliyo karibu na Yordani, kwa upande huo ulio milki ya wana wa Israeli. 12#Amu 20:1 Basi, wana wa Israeli waliposikia habari hiyo, mkutano wote wa wana wa Israeli wakakutanika pamoja huko Shilo, ili waende kupigana nao.
13 # Kum 13:14; Amu 20:12; Kut 6:25; Hes 25:7 Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, hadi nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani; 14#Hes 1:4 na pamoja naye wakuu kumi, mkuu mmoja wa nyumba ya mababa kutoka kwa kila kabila la Israeli; nao kila mmoja alikuwa ni kichwa cha nyumba ya mababa katika maelfu ya Israeli. 15Nao wakawafikia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena, 16#Kum 12:13-14; Law 17:8,9; 1 Sam 15:23 Mkutano wote wa BWANA wanena, Ni kosa gani hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha kumfuata BWANA, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya BWANA? 17#Hes 25:1-9; Kum 4:3 Je! Ule uovu wa Peori haututoshi, ambao hamjajitakasa nafsi zenu katika huo hata hivi leo, ijapokuwa ilikuja tauni juu ya mkutano wa BWANA, 18#Mwa 18:23,25; Hes 16:22; Yos 7:11,12; 2 Sam 1:17; 1 Nya 21:1,14 hata ikawa hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumfuata BWANA? Kisha itakuwa, kwa kuwa ninyi mnamwasi BWANA hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa Israeli. 19#Law 17:8,9; Yos 18:1 Basi ikiwa hiyo inchi yenu ni najisi, vukeni na kuingia katika nchi ya milki yake BWANA, ambamo maskani ya BWANA inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi BWANA, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wetu. 20#Yos 7:1-26; 1 Nya 2:6,7 Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?
21 # Mit 15:1; 18:3 Ndipo hapo wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wakajibu, na kuwaambia hao waliokuwa ni vichwa vya maelfu ya Israeli, wakasema, 22#Kut 15:11; Kum 10:17; Zab 82:1; Dan 2:47; Ufu 19:16; 1 Fal 8:39; Ayu 10:7; Zab 44:21; Yer 12:3; Yn 2:25; 21:17; 2 Kor 11:11,31; Ebr 4:13; Ufu 2:23 Mungu, Mungu BWANA, naam, Mungu, Mungu BWANA, yeye anajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika uasi, au kama ni katika kosa juu ya BWANA, usituokoe hivi leo; 23#Kum 18:19; 1 Sam 20:16; Zab 7:3,5; 10:13,14 kama tumejijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumfuata BWANA; au kama ni kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye BWANA mwenyewe na atulipize kisasi; 24au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hofu kuwa, katika siku zijazo wana wenu huenda wakanena na wana wetu na kusema, Ninyi mna uhusiano gani na BWANA, Mungu wa Israeli? 25Kwa kuwa yeye BWANA ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati yetu nanyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika BWANA; basi hivyo wana wenu wangeweza kuwafanya wana wetu waache kumwabudu BWANA. 26Kwa ajili ya hayo tulisema, Natujijengee madhabahu, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala kwa sadaka yoyote; 27#Mwa 31:48; Yos 24:27; 1 Sam 7:12; Kum 12:5-27 bali iwe ushahidi kati yetu nanyi, tena kati ya vizazi vyetu baada yetu, kwamba sisi tunamhudumia BWANA kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika siku zijazo, Ninyi hamna fungu katika BWANA. 28Kwa hiyo tulisema, Itakuwa, hapo watakapotuambia neno kama hilo, au kuwaambia watu wa vizazi vyetu katika siku zijazo neno kama hilo, ndipo sisi tutawaambia, Angalieni huu mfano wa madhabahu ya BWANA, walioufanya baba zetu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wala kwa ajili ya dhabihu; lakini ni ushahidi kati yetu nanyi. 29#Kum 12:13,14 Mungu na atuzuie tusimwasi BWANA, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumfuata BWANA, hata mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au dhabihu, mbali na ile madhabahu ya BWANA, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya maskani yake.
30Basi Finehasi kuhani, na wakuu wa mkutano, na hao vichwa vya maelfu ya Israeli waliokuwa pamoja naye, hapo walipoyasikia hayo maneno waliyoyasema hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, maneno hayo yaliwaridhisha sana. 31#Kut 25:8; 29:45; Law 26:11,12; 1 Fal 8:57-58; 2 Nya 15:2; Zek 8:23; 1 Kor 14:25; Ufu 21:3 Naye Finehasi, mwana wa Eleazari, kuhani, akawaambia wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, akasema, Siku hii ya leo tumejua ya kwamba BWANA yu kati yetu, kwa sababu hamkukosa katika jambo hili mbele ya BWANA; sasa ninyi mmewaokoa wana wa Israeli na mkono wa BWANA. 32Kisha Finehasi, mwana wa Eleazari, kuhani, na hao wakuu, wakarudi na kuwaacha wana wa Reubeni na wana wa Gadi, wakatoka katika nchi ya Gileadi, na kuingia nchi ya Kanaani; wakawarudia wana wa Israeli, wakawapa habari. 33#1 Nya 29:30; Neh 8:6; Dan 2:19; Lk 2:28 Ripoti hiyo ikawaridhisha Waisraeli; nao Waisraeli wakamhimidi Mungu, wala hawakusema tena habari ya kuwaendea ili kupigana nao, wala kuiharibu nchi waliyoikaa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi. 34#Yos 24:27 Basi hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakaiita madhabahu hiyo Edi; wakasema, Kwa kuwa ni ushahidi kati yetu ya kwamba yeye BWANA ndiye Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Yoshua 22: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha