Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 17

17
Nusu nyingine ya kabila la Manase (magharibi)
1 # Mwa 41:51; 48:18; 50:23; Kum 3:15 Hii ndiyo sehemu waliyopewa kabila la Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Na Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani. 2#Hes 26:29-32; 1 Nya 7:18 Na kura ilikuwa ni ya hao wana wa Manase waliosalia kwa kufuata jamaa zao; kwa wana wa Abiezeri, kwa wana wa Heleki, kwa wana wa Asrieli, kwa wana wa Shekemu, kwa wana wa Heferi na kwa wana wa Shemida; hao ndio wana wa kiume wa Manase, mwana wa Yusufu, kwa kufuata jamaa zao. 3#Hes 26:33; 27:1; 36:2 Lakini Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, hakuwa na wana wa kiume ila binti; na majina ya hao binti zake walikuwa wakiitwa Mala, Nuhu, Hogla, Milka na Tirza. 4#Hes 27:1-7; Yos 14:1 Nao wakaja mbele ya kuhani Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya viongozi, wakasema, BWANA alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuifuata hiyo amri ya BWANA akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao. 5Kisha kura zilizomwangukia Manase zilikuwa ni sehemu kumi, mbali na nchi ya Gileadi na Bashani, iliyo ng'ambo ya Yordani; 6#Hes 26:29; 32:39,41 kwa sababu hao binti za Manase walikuwa na urithi katika wanawe wa kiume; na nchi ya Gileadi ilikuwa ni mali ya hao wana wa kiume wa Manase waliosalia. 7Mpaka wa Manase ulikuwa kutoka Asheri hadi Mikmeta, ulioelekea Shekemu; tena mpaka ukaendelea upande wa kulia, hata kuwafikia wenyeji wa Entapua. 8#Yos 12:17; 15:34 Hiyo nchi ya Tapua ilikuwa ni mali ya Manase; lakini ule mji wa Tapua uliokuwa katika mpaka wa Manase ulikuwa ni mali ya wana wa Efraimu. 9#Yos 16:8,9 Tena mpaka uliteremka hadi kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na mwisho wake ulikuwa baharini; 10upande wa kusini ilikuwa ni mali ya Efraimu, na upande wa kaskazini ilikuwa ni mali ya Manase, na bahari ilikuwa mpaka wake; nao wakafika hadi Asheri upande wa kaskazini, na kufika hata Isakari upande wa mashariki. 11#Yos 16:9; 1 Nya 7:29; 1 Sam 31:10; 1 Fal 4:12 Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Beth-sheani na vijiji vyake, Ibleamu na miji yake, wenyeji wa Dori na miji yake, wenyeji wa Endori na miji yake, wenyeji wa Taanaki na miji yake, wenyeji wa Megido na miji yake, na pia theluthi ya Nafathi. 12#Amu 1:27-28; Kut 23:29-33; Hes 33:52 Lakini wana wa Manase hawakuweza kuwafukuza wenyeji wa miji hiyo; bali hao Wakanaani walijikaza ili wakae katika nchi hiyo. 13#Yos 16:10 Kisha ikawa, hapo hao wana wa Israeli walipokuwa wamepata nguvu zaidi, ndipo wakawalazimisha hao Wakanaani wafanye kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa.
Kabila la Yusufu lateta
14 # Yos 16:4; Mwa 48:22; 48:19; Hes 26:34,37 Kisha wana wa Yusufu wakanena na Yoshua, wakasema, Kwa nini umenipa mimi sehemu moja tu na fungu moja kuwa ni urithi wangu, kwa kuwa mimi ni taifa kubwa la watu, kwa sababu BWANA amenibariki hata hivi sasa? 15Yoshua akawaambia, Kwa kuwa wewe u taifa kubwa la watu, haya, kwea uende mwituni, ujikatie mahali hapo kwa ajili ya nafsi yako katika nchi ya Waperizi, na ya hao Warefai; maana hiyo nchi ya vilima ya Efraimu ni nyembamba, haikutoshi. 16#Amu 1:19; 4:3; Yos 19:18; Amu 6:33; 1 Fal 4:12; 18:46 Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Beth-sheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia. 17Kisha Yoshua alinena na nyumba ya Yusufu, maana, ni Efraimu na Manase, akawaambia, Wewe u taifa kubwa la watu, nawe una uwezo mwingi; hutapata sehemu moja tu; 18#Kum 20:1; Yos 11:4-6; 13:6; Rum 8:31; Ebr 13:6 lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa sasa ni msitu, wewe utaufyeka, na kuimiliki yote hadi mwisho wake; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.

Iliyochaguliwa sasa

Yoshua 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia