Yoeli 2
2
1 #
Hes 10:5; Zab 87:1; Oba 1:15; Sef 1:14 Pigeni tarumbeta katika Sayuni,
Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu;
Wenyeji wote wa nchi na watetemeke;
Kwa maana siku ya BWANA inakuja.
Kwa sababu inakaribia; 2#Amo 5:18; Yoe 1:6; Kut 10:14 siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
3 #
Zek 7:14
Moto unaunguza vikali mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Edeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao. 4#Ufu 9:7-9 Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopiga mbio. 5Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto iunguzapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. 6#Yer 8:21 Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu. 7Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao. 8Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake; huendelea mbele kila mmoja katika njia yake; hujifanyia njia kwa nguvu kati ya silaha, wala hawaachi kuifuata njia yao. 9Huurukia mji; hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama aingiavyo mwizi. 10#Ufu 8:12 Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza; 11#Yer 50:34; Hes 24:23; Mal 3:2; Ufu 6:17 naye BWANA anatoa sauti yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?
12 #
Yer 4:1; Hos 12:6 Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza; 13#2 Fal 22:19; Zab 34:18; Isa 57:15; Mt 5:3,4; Kut 34:6; Yon 4:2 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi kuadhibu. 14#Yos 14:12; Sef 2:3; Isa 65:8; Hag 2:19 Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?
15Pigeni tarumbeta katika Sayuni,
Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;
16 #
Kut 19:10; 2 Nya 20:13; 1 Kor 7:5 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko,
Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto,
Na hao wanyonyao maziwa;
Bwana arusi na atoke chumbani mwake,
Na bibi arusi katika hema yake.
17 #
Mt 23:35; Kut 32:11; Isa 37:20 Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie
Kati ya patakatifu na madhabahu,
Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA,
Wala usiutoe urithi wako upate aibu,
Hata mataifa watawale juu yao;
Kwa nini waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Majibu ya Mungu na ahadi yake
18 #
Isa 42:13; Zek 1:14; Kum 32:36; Zab 103:13 Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake. 19#Mal 3:10 BWANA akajibu, akawaambia watu wake; Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa; 20#Kut 10:19; Kum 11:24 lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa.
21 #
1 Yoh 4:18
Ee nchi, usiogope; furahi na kushangilia; kwa kuwa BWANA ametenda mambo makuu. 22#Zek 8:12 Msiogope, enyi wanyama wa porini; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. 23#Zab 28:7; Isa 12:2-6; Hab 3:17,18; Zek 10:7; Law 26:4; Yak 5:7 Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama awali. 24Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. 25Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. 26#Mik 6:14 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. 27#Law 26:11; Isa 45:5 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Roho wa Mungu amiminiwa
28 #
Isa 44:3; Yn 7:39; Isa 54:13; Mdo 2:17-21; 21:9 Hata#2:28 Katika Kiebrania ni Sura 3:1. itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, wa kiume na wa kike, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29#1 Kor 12:13; Gal 3:28 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. 30#Mk 13:24 Nami nitaonesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. 31#Mt 24:29; Mk 13:24-25; Lk 21:25; Ufu 6:12-13 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo. 32#Zab 50:15; Yer 33:3; Mdo 2:21; 1 Kor 1:2; Isa 46:13; 11:11; Oba 1:17; Rum 10:13; 9:27 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.
Iliyochaguliwa sasa
Yoeli 2: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.