Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 4:3-8

Ayubu 4:3-8 SRUV

Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge. Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge. Lakini sasa haya yamekufikia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika. Je! Dini yako siyo tegemeo lako? Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali? Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.

Soma Ayubu 4