Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 4:3-8

Ayu 4:3-8 SUV

Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge. Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge. Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika. Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi? Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.