Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 33:8-22

Ayubu 33:8-22 SRUV

Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema, Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu; Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake; Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza. Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. Kwa nini unapingana naye, ukisema, Hatajibu hata neno langu moja? Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ijapokuwa mtu hatambui. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia mhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokeza nje. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.

Soma Ayubu 33