Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 12

12
Ayubu ajibu: Mimi nachekwa sana
1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2Hapana shaka ninyi ndinyi watu halisi,
Nanyi mtakapokufa, ndipo na hekima itakoma.
3Lakini mimi pia, nina fahamu kama ninyi;
Mimi si duni kuliko ninyi;
Naam, ni nani asiyejua mambo kama hayo?
4 # Ayu 16:20; Zab 91:15; Yer 33:3; Mik 7:7 Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake,
Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu;
Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko.
5 # Mit 14:2 Katika mawazo yake huyo aliye na raha mna kudharau balaa;
Tayari kwa ajili ya wenye kuteleza miguu.
6Hema za wanyang'anyi hufanikiwa,
Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama;
Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.
7Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha;
Na ndege wa angani, nao watakuambia;
8Au nena na nchi, nayo itakufundisha;
Nao samaki wa baharini watakutangazia.
9Katika hawa wote ni yupi asiyejua,
Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya?
10 # Hes 16:22; Dan 5:23; Mdo 17:28 Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake,
Na pumzi zao wanadamu wote.
11Je! Sikio silo lijaribulo maneno,
Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?
12Wazee ndio walio na hekima,
Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.
13Hekima na amri zina yeye [Mungu];
Yeye anayo ushauri na fahamu.
14 # Ufu 3:7 Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena;
Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
15 # 1 Fal 17:1; Mwa 7:11 Tazama, yuayazuia maji, nayo yakatika;
Tena, huyatuma, nayo yaipindua dunia.
16Kwake yeye ziko nguvu, na hekima;
Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.
17Yeye huwaondoa washauri wakiwa wamevuliwa nguo,#12:17 au wametekwa nyara.
Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.
18Yeye hulegeza kifungo cha wafalme,
Na kuwafunga viuno vyao kwa mshipi.
19Yeye huwaondoa makuhani wakiwa wamevuliwa nguo.
Na kuwapindua mashujaa.
20Huondoa usemi wa hao walioaminiwa,
Na kuondoa fahamu za wazee.
21Humwaga aibu juu ya hao wakuu,
Na kulegeza mshipi wa wenye nguvu.
22 # Mt 10:26; 1 Kor 4:5 Huvumbua mambo ya siri tokea gizani,
Na hicho kilicho giza tupu huleta mwangani.
23Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza;
Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha.
24Huwaondolea moyo wakuu wa watu wa nchi,
Na kuwapoteza nyikani pasipokuwa na njia.
25Wao hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga,
Naye huwafanya kupepesuka kama mlevi.

Iliyochaguliwa sasa

Ayubu 12: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia