Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 6:16-21

Yohana 6:16-21 SRUV

Hata ilipokuwa jioni wanafunzi wake wakateremka baharini wakapanda katika mashua, wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaumu. Nako kumekwisha kuwa giza, wala Yesu hajawafikia. Na bahari ikaanza kuchafuka kwa kuvuma upepo mkuu. Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kuikaribia mashua; wakaogopa. Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. Basi wakataka kumpokea katika mashua; na mara hiyo mashua ikaifikia nchi waliyokuwa wakiiendea.

Soma Yohana 6

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yohana 6:16-21