Yeremia 51:60-62
Yeremia 51:60-62 SRUV
Naye Yeremia akaandika katika kitabu kuhusu mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli. Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote, ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.