Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 49

49
Hukumu juu ya Waamoni
1 # Eze 21:28-32; 25:1-7; Amo 1:13-15; Sef 2:8-11 Kuhusu wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake? 2#Amo 1:14 Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya kishindo cha vita kisikike juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema BWANA.
3 # Isa 32:11; Yer 48:7 Omboleza, Ee Heshboni,
Kwa maana Ai umeangamizwa;
Lieni, enyi binti za Raba,
Mjivike nguo za magunia;
Ombolezeni, mkipiga mbio
Huko na huko kati ya maboma;
Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa,
Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
4 # Yer 21:13 Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijia? 5Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, BWANA wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao. 6#Yer 48:47 Lakini baada ya hayo nitawarudisha wana wa Amoni walio utumwani, asema BWANA.
Hukumu juu ya Edomu
7 # Amo 1:11; Ayu 5:12-14; Oba 1:8; Isa 19:11 Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao? 8#Isa 2:19; Yer 25:23 Kimbieni, rudini nyuma, kaeni chini sana, enyi mnaokaa Dedani; maana nitaleta msiba wa Esau juu yake, wakati nitakapomwangalia. 9#Isa 17:6 Je! Kama wachuma zabibu wangekujia, wasingeacha zabibu ziokotwe? Kama wangekujia wezi usiku, wasingeharibu hata watakapopata vya kutosha? 10#Isa 17:14 Lakini nimemwacha akiwa hana kitu Esau, nimepafunua mahali pake pa siri, wala hataweza kujificha; kizazi chake kimeangamizwa, na ndugu zake, na jirani zake, naye mwenyewe hayuko. 11Waache watoto wako wasio na baba, mimi nitawahifadhi hai, na wajane wako na wanitumaini mimi. 12#Yer 25:29; Oba 1:16 Maana BWANA asema hivi, Tazama, wale wasioandaliwa kunywea kikombe, watakinywea, ni hakika; na wewe je! U mtu ambaye hataadhibiwa kabisa? Hukosi utaadhibiwa, naam, kunywa utakunywa. 13#Mwa 22:16; Isa 45:23; 34:6; Amo 6:8; 1:12 Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
14 # Oba 1:1,2 Nimepata habari kwa BWANA,
Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa,
Akisema, Jikusanyeni, mkaujie,
Mkainuke kwenda vitani.
15Maana nimekufanya mdogo kati ya mataifa,
Na kudharauliwa katika watu.
16 # Ayu 39:27; Mit 15:25; Amo 9:2 Kuhusu kuogofya kwako,
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,
Wewe ukaaye katika pango za majabali,
Ushikaye kilele cha milima;
Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai,
Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
17 # Yer 18:16; 50:13 Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote. 18#Mwa 19:24-25; Kum 29:23; Yer 50:40; Amo 4:11 Kama vile vilivyotokea wakati wa kuangushwa Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo. 19#Yer 4:17; 12:5; Zek 11:3; Kut 15:11; Zab 89:6-8; Ayu 41:10 Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
20 # Yer 50:45 Basi, lisikieni shauri la BWANA;
Alilolifanya juu ya Edomu;
Na makusudi yake aliyoyakusudia
Juu yao wakaao Temani;
Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi;
Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
21Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao;
Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu.
22 # Yer 4:13 Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.
Hukumu juu ya Dameski
23 # Isa 17:1-3; Amo 1:3-5; Zek 9:1 Kuhusu Dameski.
Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia;
Maana wamesikia habari mbaya;
Wameyeyuka kabisa;
Wamesumbuka kama bahari, isiyoweza kutulia.
24 # Isa 13:8 Dameski umedhoofika;
Umejigeuza kukimbia; tetemeko limeushika;
Dhiki na huzuni zimeupata,
Kama za mwanamke katika uchungu wake.
25 # Yer 51:41 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu? 26Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia zake kuu, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi. 27#Amo 1:4; 2 Fal 13:3 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.
Hukumu juu ya Kedari na Hazori
28 # Ayu 1:3 Kuhusu Kedari, na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alizipiga. BWANA asema hivi, Ondokeni, pandeni hadi Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki. 29#Zab 120:5 Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia wao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote. 30Kimbieni ninyi, nendeni mbali mkitangatanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema BWANA; maana Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu. 31#Hes 23:9; Kum 33:28; Amu 18:28; Mik 7:14 Ondokeni, pandeni hata taifa lililo katika hali ya raha, likaalo bila kuhangaika, asema BWANA; wasio na malango wala makomeo, wakaao peke yao. 32#Kum 28:64; Eze 5:10; Yer 25:23 Na ngamia wao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya katika pande zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema BWANA. 33#Yer 9:11; Mal 1:3 Na Hazori utakuwa kao la mbwamwitu; ukiwa milele; hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.
Hukumu juu ya Elamu
34 # Mwa 10:22; Yer 25:25 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, juu ya Elamu, mwanzo wa kumiliki kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, kusema, 35#Mwa 14:1; Ezr 4:9; Isa 21:2; Dan 8:2 BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama nitauvunja upinde wa Elamu, ulio mkuu katika nguvu zao. 36Na juu ya Elamu nitazileta pepo nne, toka pembe nne za mbinguni, nami nitawatawanya katika pande zote nne, wala hakuna taifa ambalo hawatalifikia watu wa Elamu waliofukuzwa. 37#Yer 48:2 Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema BWANA; nami nitautuma upanga uwafuatie, hadi nitakapowaangamiza; 38#Yer 43:10; Dan 7:9 nami nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu, nami nitawaharibu, mfalme na wakuu, watoke huko, asema BWANA. 39Lakini itakuwa, katika siku za mwisho, nitawarudisha wafungwa wa Elamu, asema BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Yeremia 49: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia