Yeremia 47
47
Hukumu juu ya Wafilisti
1 #
Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza. #Isa 14:29-31; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7
2 #
Isa 8:7; Yer 1:14 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza. 3#Nah 3:2 Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu; 4#Yer 25:22; Yoe 3:4; Amo 1:9,10; 9:7; Mwa 10:14 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
5 #
Sef 2:4
Upaa umeupata Gaza;
Ashkeloni umenyamazishwa
Mabaki ya bonde lao;
Hata lini utajikatakata?
6 #
Eze 21:3
Ee upanga wa BWANA,
Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?
Ujitie katika ala yako;
Pumzika, utulie.
7 #
1 Sam 3:12; Mik 6:9 Utawezaje kutulia,
Ikiwa BWANA amekupa agizo?
Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,
Ndipo alipoyaamuru hayo.
Iliyochaguliwa sasa
Yeremia 47: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.