Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waamuzi 7

7
Gideoni awashinda Wamidiani
1 # Amu 6:32; 1 Sam 12:11; Mwa 22:3; Yos 3:1; 6:12; Mhu 9:10; Mwa 12:6 Kisha Yerubaali, yaani Gideoni, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaondoka asubuhi na mapema, wakapiga kambi yao karibu na kijito cha Harodi; na kambi ya Midiani ilikuwa upande wao wa kaskazini, karibu na mlima wa More, bondeni.
2 # Kum 8:17; 9:4; 32:27; 1 Sam 17:47; Zab 33:16-18; 44:6,7; Mit 25:6; Mhu 9:11; Isa 10:13; Yer 9:23,24; Zek 4:6; Rum 3:27; 1 Kor 1:29; 4:7; 2 Kor 4:7; 10:17; Efe 2:9 BWANA akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno kwangu kuwatia Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa. 3#Kum 20:8 Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu yeyote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu elfu ishirini na mbili wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi.
4 # 1 Sam 16:6,7 BWANA akamwambia Gideoni; Hata sasa watu hawa ni wengi mno; walete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako; kisha itakuwa ya kwamba yule nitakayekuambia, Huyu atakwenda pamoja nawe, ndiye atakayekwenda pamoja nawe; na mtu yule nitakayekuambia, Huyu hatakwenda pamoja nawe, basi mtu huyo hatakwenda. 5Basi akawaleta watu chini majini. BWANA akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa. 6Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji. 7#1 Sam 14:6; Isa 41:14,18 BWANA akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake. 8Basi Gideoni akachukua vyakula vyao na tarumbeta zao, kisha akawaaga watu wote wa Israeli, kila mtu hemani mwake; akabaki na watu mia tatu; na kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake, bondeni.#7:8 Katika Kiebrania ni ‘wale watu’.
9 # Mwa 46:2,3; Ayu 4:13; Mt 1:20; Mdo 18:9,10; 27:23 Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako. 10Lakini, ukiogopa kushuka, shuka pamoja na Pura mtumishi wako kambini; 11#Mwa 24:14; 1 Sam 14:9,10 nawe utasikia wanayoyasema, na baada ya haya, mikono yako itatiwa nguvu; ushuke kambini. Ndipo akashuka pamoja na Pura mtumishi wake hadi katika vituo vya walinda zamu wa kambi ya Wamidiani. 12#Amu 6:5,33; 8:10 Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia wao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi. 13#Amu 6:15; Isa 41:14,15; 1 Kor 1:27 Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, niliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika katika hema moja, ukaipiga hadi ikaanguka, ukaipindua, hadi ikalala chini. 14#Mwa 40:8; Hes 23:5 Mwenzake akamjibu akasema, Habari hii haikosi kuwa upanga wa Gideoni, mwana wa Yoashi, mtu wa Israeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote katika mkono wake. 15Ikawa, aliposikia habari ya ile ndoto, na kufasiriwa kwake, akasujudu; akarudi katika jeshi la Israeli akasema, Inukeni, kwa maana BWANA amelitia jeshi la Midiani mikononi mwenu. 16#Hes 10:9; Yos 6:4; 2 Nya 13:14,15; Amo 3:6 Kisha akawapanga wale watu mia tatu wawe vikosi vitatu, akatia tarumbeta katika mikono ya watu wote, na mitungi isiyo na maji, na mienge ndani ya hiyo mitungi. 17Akawaambia, Nitazameni, mkafanye kama nifanyavyo mimi; angalieni, nitakapofika mwisho wa kambi, itakuwa, nifanyavyo mimi nanyi fanyeni vivyo hivyo. 18Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa BWANA, na kwa Gideoni.
19 # Kut 14:24; Lk 12:38; Ufu 16:15 Basi Gideoni, na wale watu mia moja waliokuwa pamoja naye, wakafika mwisho wa kambi, mwanzo wa zamu ya kati, wakati walipokuwa wamebadili wenye zamu; wakazipiga hizo tarumbeta, wakaivunja vipande vipande ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao. 20Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa BWANA na wa Gideoni. 21#Kut 14:13,14,25; 2 Nya 20:17; Isa 30:7,15; 2 Fal 7:7; Ayu 15:21,22; Mit 28:1 Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote; jeshi lote wakakimbia; nao wakapiga kelele, wakawakimbiza. 22#Yos 6:4,16,20; 2 Kor 4:7; 1 Sam 14:20; Zab 83:9; Isa 9:4; 19:2; 2 Nya 20:23 Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuelekea Serera, hadi mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi. 23Wanaume wa Israeli walikuwa wamekusanyika kutoka Naftali, na kutoka Asheri, na kutoka Manase yote, wakawafuata Midiani. 24#Amu 3:27; Rum 15:30; Flp 1:27; Amu 3:28; Yn 1:28 Kisha Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, teremkeni juu ya Midiani, na kuyatwaa hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana huo mto wa Yordani. Basi wanaume wote wa Efraimu walitokeza wakayatwaa maji mpaka Bethbara, yaani, huo mto wa Yordani. 25#Amu 8:3,4; Zab 83:11; Isa 10:26 Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng'ambo ya pili ya Yordani.

Iliyochaguliwa sasa

Waamuzi 7: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia