Isaya 51:17-23
Isaya 51:17-23 SRUV
Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza. Hapana hata mmoja wa kumwongoza Miongoni mwa wana wote aliowazaa, Wala hapana hata mmoja wa kumshika mkono Miongoni mwa wana wote aliowalea. Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza? Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya BWANA, Lawama ya Mungu wako. Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo; BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena; nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.