Isaya 42
42
Mtumishi nuru kwa mataifa
1 #
Isa 49:3,6; 52:13; Mt 3:17; 12:18; 17:5; Flp 2:7; Yn 3:35; Efe 1:6; Kol 1:12-14; Isa 11:2; Mk 1:11; Lk 3:22; 9:35 Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. 2Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. 3Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu. 4#Ebr 12:2; Mwa 49:10 Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. 5#Isa 44:24; Zek 12:1; Mdo 17:25 Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake. 6#Isa 49:6; Lk 2:32; Mdo 13:47; 26:23 Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; 7#Lk 4:18; 2 Tim 2:26; Ebr 2:14; Isa 9:2 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. 8#Kut 3:14; Isa 48:11 Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. 9Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.
Wimbo wa sifa
10 #
Zab 33:3; 40:3; 107:23 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Na sifa zake tokea mwisho wa dunia;
Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo,
Na visiwa, nao wakaao humo.
11Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao,
Vijiji vinavyokaliwa na Kedari;
Na waimbe wenyeji wa Sela,
Wapige kelele toka vilele vya milima.
12Na wamtukuze BWANA,
Na kutangaza sifa zake visiwani.
13BWANA atatokea kama shujaa;
Ataamsha wivu kama mtu wa vita;
Atalia, naam, atapiga kelele;
Atawatenda adui zake mambo makuu.
14Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja. 15Nitaharibu milima na vilima, nitavikausha vyote vimeavyo; nitaifanya mito ya maji kuwa visiwa, na kuyakausha maziwa ya maji. 16Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha. 17Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu.
18Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona. 19#Isa 43:8; Eze 12:2; Yn 7:49 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA? 20#Kum 4:3; Isa 1:3; Rum 2:21 Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake yako wazi, lakini hasikii.
Uasi wa Israeli
21BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. 22Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. 23Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao? 24Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosea, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake. 25#2 Fal 25:9; Hos 7:9 Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake.
Iliyochaguliwa sasa
Isaya 42: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.