Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 33

33
Unabii wa kukombolewa kutoka kwa watesi
1 # Hab 2:8; Ufu 13:10 Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe. 2Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu#33:2 Au, mkono wao. kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu. 3Makabila ya watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako. 4Na mateka yako yatakukusanywa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige. 5#Zab 97:9 BWANA ametukuka; kwa maana anakaa juu; amejaza Sayuni hukumu na haki. 6#Mit 1:7; Mt 6:33 Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.
7 # 2 Fal 18:18 Angalia, mashujaa wao wanalia nje, wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu. 8#Amu 5:6; 2 Fal 18:14 Njia kuu zimeachwa, msafiri ameikimbia barabara; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu. 9Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani. 10#Kum 32:36,43; Zab 12:5; Isa 42:13,14; Sef 3:8 Basi, sasa nitasimama; asema BWANA; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza. 11Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe. 12Nao mataifa watakuwa kama kuchoma chokaa, kama miiba iliyokatika, iteketezwayo motoni.
13Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uwezo wangu. 14Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele? 15Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu. 16Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Nchi ya mfalme mkuu
17Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana. 18#1 Kor 1:20 Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara? 19#Yer 5:15 Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuielewa. 20Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika. 21#Zek 2:5 Bali huko BWANA atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo. 22#Zab 44:4; Mt 21:5; Ufu 19:16 Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa. 23Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka. 24#Isa 12:2; Rum 11:27 Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 33: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia