Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 20

20
Isaya aigiza kushindwa kwa Misri na Kushi
1 # 2 Fal 18:17 Katika mwaka ule jemadari#20:1 Jemadari hapa, kwa Kiebrania ni Tartan. yule alipofika Ashdodi, alipotumwa na Sargoni mfalme wa Ashuru; naye alipigana na Ashdodi akautwaa; 2#Zek 13:4; 1 Sam 19:24 wakati huo BWANA alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako. 3#Isa 8:18 Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake ikiwa haina viatu. BWANA akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, bila viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya Kushi; 4#2 Sam 10:4; Mik 1:11 vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, bila viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe. 5#2 Fal 18:21; Isa 31:1-3 Nao watafadhaika, na kuona haya kwa ajili ya Kushi, matumaini yao, na Misri, utukufu wao. 6Na mwenyeji wa nchi ya pwani atasema katika siku hiyo, Angalia, haya ndiyo yaliyowapata watu wale tuliowatumainia, ambao tuliwakimbilia watuokoe kutoka kwa mfalme wa Ashuru; na sisi je! Twawezaje kupona?

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 20: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia